Serikali Yaanza Kuwashughulikia Wasanii Wanaovaa Nusu UCHI....Tazama Majina ya Baadhi Yao

Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema
kuwa, serikali inafuatilia kwa karibu wasanii wote wanaoweka picha za
kukosa maadili kwenye mitandao na kuwachukulia hatua.
Shonza
ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaama alipokuwa akizungumza na
vyombo vya habari. Agizo hilo la Naibu Waziri ni matokeo ya kauli
iliyotolewa na Rais Dkt Magufuli aliyoitoa mjini Dodoma wakati
akizungumza na Jumuiya ya Wazazi ya CCM.
Rais
Magufuli alivitaka vyombo husika kuwachukulia hatua wasanii hasa wa
kike ambao wamekuwa wakivaa nguo zinazopelekea kumomonyoka kwa maadili.
Wakati
akizungumza hayo Naibu Waziri alitaja majina ya wasanii ambao wameanza
kuwachukulia hatua ambapo baadhi wametakiwa kufika ofisini kwake huku
mwingine akifungiwa kujihusisha na masuala ya sanaa kwa muda wa miezi
sita.
Shonza
amemtaka msanii, Jane Rimoy maarufu kwa jina la Sanchi kufika ofisini
kwake mara moja kutokana na kuchapisha mitandaoni picha zisizo na
maadili.
Mbali
na Sanchi, Shonza ametoa maagizo, ”Ninamtaka Msanii wa Bongo Fleva,
Gift Stanford maarufu kama Gigy Money kufika ofisini kwangu mara moja
sababu alitumiwa ujumbe lakini hakujibu, hivyo ajue kuwa hawezi
kushindana na serikali.”
Pia,
Naibu Waziri wa Habari, Juliana Shonza amemfungia msanii wa filamu na
muziki, Suzan Michael maarufu Pretty Kind kujihusisha na shughuli zote
za sanaa kwa muda wa miezi sita, kutokana na kuweka picha za utupu
katika mtandao ya kijamii.
Wakati
huo huo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey
Mngereza amewasisitiza wamiliki wa studio za kutayarisha kazi za sanaa
na waandaji wa kazi za sanaa (Producers) kujisajili katika ofisi za
Baraza hilo. Asisitiza, kufanya kazi bila kusajiliwa ni kinyume na
sheria.
Source: Mpekuzi HuruRead More
No comments