Saa zahesabika msako wa mtuhumiwa kifo cha mke

Jeshi
la Polisi limesema msako dhidi ya Mhasibu wa Hospitali ya Rufaa ya
Mbeya, Ami Lukule, ambaye anatuhumiwa kwa mauaji ya mkewe, kichanga
chake na shemejiye wa kike, unaendelea vizuri na wanaamini kuwa watamtia
mbaroni wakati wowote.
Lukule
anadaiwa kutekeleza mauaji hayo kwa kutumia jembe la kulimia Jumatano
iliyopita, katika eneo la Masota Darajani, Goba jijini Dar es Salaam.
Waliofariki kutokana na tukio hilo ni Pendo Lukule, kichanga chake cha
umri wa miezi minne, Joshua na shemeji wa kike wa mtuhumiwa ambaye ni
ndugu wa mkewe, Magreth Samwel.
Inadaiwa
kuwa Lukule alikimbilia kusikojulikana mara tu baada ya kufanikisha
mauaji hayo, huku akiacha ujumbe unaowataka polisi kutohangaika kwa
sababu ni yeye aliyetekeleza mauaji kutokana na kitendo cha mkewe
kutokuwa mwaminifu na kwamba hata mtoto aliyemuua siyo wa kwake bali
mkewe amezaa na watu wengine.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benedict Kitalika,
amesema kuwa hadi sasa, wanaendelea vizuri na msako dhidi ya mtuhumiwa
kwa sababu wameshapata taarifa muhimu za kumtia mbaroni wakati wowote
kuanzia sasa.
“Tumeshapokea
taarifa na tunaamini zitatusaidia kumpata… yupo hapa nchini. Jeshi letu
lipo vizuri, tutamkamata na kumchukulia hatua dhidi ya mauaji
aliyoyafanya,” amesema Kitalika.
Katika hatua nyingine, taarifa zilidai jana kuwa miili ya marehemu inatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni.
Source: Mpekuzi HuruRead More
No comments