12 important things Diamond and Rayvanny told Basata in their open letter protesting the ban on their song
Diamond Platnumz and Rayvanny won’t take Basata’s ban on their new song lying down. The Tanzanian music regulatory body banned ‘Mwanza’ on grounds that has explicit sexual content.
Rayvanny and Diamond have both written an open letter to Basata protesting the ban on their song. The two singers both relayed a 6 point message to Basata.
For Diamond, he cited several reasons protesting the blanket ban on the new song, he explained that; Mwanza is not targeting kids, pulling down Mwanza from YouTube was inappropriate since the song is not only for Tanzanian audience, he also said that he will lose revenue from the ban of Mwanza.
KWA WAZEE WANGU WA BARAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA)Kwanza kabisa niwapongeze kwa kazi nzito na nzuri Mnayoifanya, lakini pia niwape pole kwa changamoto mbalimbali mnazokutana nazo, maana najua ugumu mnaopitia katika kusimamia sanaa yetu Nchini.Ujumbe wenu kuhusu kufungiwa wimbo wa #Mwanza almaarufu kama #NYEGEZI wakuu nimeupata ila tu kwabahati mbaya mtoto wenu niko Canada katika harakati za kutafta rizki ili kuendelea kulijenga taifa na kuendelea kutangaza sanaa zetu, ila laiti ningelikuwa nchini ningekujamara moja kama mnavyonijuaga pindi mniitapo basi hufika haraka bila ukaidi.Tukiwa kama Wasani ambao tumesajiliwa, tuna kila haki ya kuheshimu na kutii baraza letu la sanaa BASATA pindi linapotoa tamko, kwa sababu wao ndio wazazi na walezi wetu kwenye hii sanaa, na kwa kutambua kuwa Sanaa ni kazi ya Ubunifu, na kwenye kubuni wakati mwingine kuna kuwa na usawa na wakati mwingine kutokuwa sawa.Ndiyo maana mliteuliwa nyinyi wazee wetu maalum kwa jili ya kuhakikisha wasanii wanapotoka nje ya Mstari mnawarudisha ili tuwe na sanaa ilio bora, tuzidi kufanikiwa, na kukua vyema na hata wasanii, mashabiki pamoja na taifa kwa ujumla lijivunie na linufaike na sanaa.Ila Kwenye UFUNGIWAJI huu nami nilikuwa nina OMBI ama PENDEKEZO kwa balaza letu pendwa la sanaa Tanzania (BASATA).Licha ya kuwa ni kweli #NYEGEZI ni eneo na Kituo cha Mabasi kilichopo MWANZA, lakini pia ni vyema kama balaza letu pendwa la sanaa kutambua pia kuwa sio kila nyimbo ni kwa ajili ya watoto wadogo. Hivyo kusema isipigwe kwenye TV na Radio tumekubali, lakini iwe kwenye Ule muda ambao serikali uliuweka wa kuwa watoto wako macho, ila pale wanapolala, basi uruhusiwe ili walengwa wautazame.PILI:- Kusema tuifute Mitandaoni pia, naomba pia Baraza letu pendwa litutazame pia na hapo. Kwa sababu mtoto mdogo tunaemlenga kumlinda asiharibikiwe kimaadili hapa, sizani kama mzazi wake anaweza kumruhusu akaperuziperuzi bila mipaka mitandaoni maana kama kweli ana uwezo wa kufanya hivyo basi anauwezo wa kwenda kuangalia hata Video za utupu, na vitu vingine ambayo wote tunafahamu ndio hatari na Madhara zaidi kwa watoto, kuliko hichi kinyimbo chetu cha MWANZA NYEGEZI.Wazee wetu, vijana wenu ama wasanii wenu sasahivi tumefanikiwa kuingia kwenye masoko mbalimbali hivyo sio kila nyimbo ni kwajili ya soko la nyumbani Tanzania tu, mfano: UGANDA kuna Tamasha Linaitwa NYEGE FESTIVAL.Na kwa nafasi niliyonayo UGANDA na kwajinsi nyimbo hii ilivyovuma kwa kishindo kila kona ndani ya siku tatu tu Viewers 1.5+ Millions Youtube, basi naamini kabisa Mwakani lazima NYEGE FETIVAL waniite kutumbuiza, na kama mnavyofahamu bei zangu huwaga si chini dola elf Sabini za Kimarekani ($70,000) kwa show sawa na milioni (160,300,000 za Kitanzania)….. ambazo kwa show moja tu ningeweza kuchangia pato la kodi si chini ya milioni (48,090,000 ya Kitanzania), hivyo naomba mlitazame na hapo Baraza letu Pendwa.NNE:- Pia ikija Upande wa Kuitumbwiza stejini naomba pia mlitazame zaidi…Maana show zetu zote ni za Usiku wa manane ambapo watoto wamelala majumbani Tunaowaimbia ni Watu wazima…
na hata #WasafiFestival2018 pia ifikapo saa 12 jioni ni wenye Umri wa zaidi ya miaka 18 tu….hivyo tutaowaimbia ni watu wazima tu.TANO:- Wazee wangu wa Balaza la sanaa BASATA nilikuwa naomba Muipe sikio tena Nyimbo pale kwenye kipande cha Amber Rutty.. kwasababu Ujumbe wangu pale ni kupingana na kile kitendo, na ndiomaana nikasema “kananivuta ghetto nikapige Bunduki, ila naogopa Centro Michezo ya Amber Rutty” Sasa hapo ubaya wake uko sehem gani…maana naamini kupitia mstari huo utakuwa ni kama Kumbusho kwa kijana ama mtuyoyote kuwa “usidiriki kufanya, Utapelekwa jela.” sasa hapo wapi ubaya wake wazee wetu.SITA:- wazee wangu wa Basata ni siku tatu tu Tangu kutoka kwa wimbo huu, lakini kika Mwana Africa na hata asiekuwa Mwana Africa Ashapajua Nyegezi Mwanza, na naamini kulikuwa na wengi pengine hawapajui lakini kupitia wimbo Huu sasa wamepajua, na naamini wengi wanatamani hata wafike, Wapigepicha, wakapashangae kuwa kumbe #NYEGEZI kwenyewe ndio hapa, na hio ndio miongoni mwa faida ya kazi ya sanaa wazee wetu.Mie yangu yalikuwa ni hayo tu, naamini Kwa Uelewa wenu na Upendo wenu mlionao kwa sanaa na wasanii wenu, mtatusaidia kwa hayo maombi yetu vijana wenu. Shukran.Ni mimi kijana wenu
Nasibu Abdul Juma
(Diamond Platnumz)
Rayvanny
For Rayvanny, he reminded Basata that being an artiste means being creative with words and not necessarily singing about things the way they are, he also talks about the song’s objective and target audience.
HABARI za asubuhi ndugu zangu, taarifa za kufungiwa kwa wimbo wangu nimezipata, lakini katika hili nina haya machache yakusema.
1.Sanaa ni nini?
Sanaa ni neno lililotokana na lugha ya kiarabu, lenye maana ya ufundi anaoutumia mwanadamu, kuwasilisha fikra au mawazo yaliyo ndani ya fikra zake, vile vile sanaa ni uzuri unaojiibua katika umbo lililosanifiwa, usanifu ni kuumba/kufanya kitu kwa kutumia ustadi ili kiweze kuvutia watu kwa uzuri wake.
Hivyo kazi yoyote ya sanaa inategemea ionyeshe ufundi wa hali ya juu, ili iwe na mvuto kwa hadhira yake iliokusudiwa, hayo maneno si yangu mimi, ni tafsiri ya neno sanaa.
2. Dhamira ya wimbo
Dhamira yetu haikua kutukana, kama inavyoonekana sasa, dhamira yetu ilikua kutoa burudani kwa hadhira iliokusudiwa ambao ni vijana wenzetu, lakini pia na mafundiosho ambayo kila siku Serikali imekua ikiyapiga vita.
3. Suala kama la Amber Rutty.
Katika wimbo wetu tumesema (nami naogopa sentro, michezo ya Amber Rutty, kwamba kijana yoyote anaesikiliza aogope kitendo hicho ataishia pabaya. Pia kuna mistari inasema (hapendagi mpasuo, hataki shida basata) ukiwa na maana ya kukataza mavazi mabaya, mavazi ya wazi nakusisitizia kwamba hata basata hayaruhusiwi. Ukiangalia haya yote ni mafundisho ambayo mwanasanaa lazima uyafikishe katika ligha iliosanifiwa.
4. Kwa nini Mwanza?
Tungeweza kuuita huu wimbo jina lingine lolote, Mbeya, Kigoma au mkoa wowote tofauti lakini kwanini Mwanza? Ikumbukwe siku chache zilizopita kumetokea maafa makubwa yaliyowakuta ndugu zetu wa Mwanza. Watu wamepoteza ndugu jamaa na marafiki.
Kama wasanii tuliwaza sana hususani kwa vijana wenzetu wa Mwanza tuwafanyie kitu gani ikiwa ni sehemu ya faraja kwao. Ndipo lilipokuja wazo la kutengeneza wimbo kwa ajili ya Mwanza. Unaosema kwetu Mwanza Nyegezi lakini tukasema usiende hivyo tu uwe na mafundisho ndani yake lakini pia burudani kwa vijana wa Mwanza na maeneo mengine. Na kiukweli wimbo huu umepokelewa vizuri sana Mwanza na maeneo mbalimbali ikiwa ni ishara ya ile dhamira tulio ikusudia imefanya kazi.
5. Kufungiwa
Kuna vyombo vya habari, na sehemu mbali mbali miziki yetu inaposikika yawezekana kukawa na watoto pengine wimbo huu haikua ni hadhira tulioikusudia. Hivyo ukisikika kwao ikawa ni kinyume na maadili kwa sababu hadhira tulioikusudia ni ya watu wazima yani miaka 18 na kuendelea.
Ambao tunaamini ndiyo wapo kwenye mitandao ya kijamii, ndiyo wanunuzi wa kazi zetu, na ndiyo wahudhuriaji wa matamasha yetu.
6. Maoni yangu
Nilikua naona suala la kufungia wimbo huu kwa vijana wenzetu ni kutunyima kufikisha ujumbe, burudani kwa hadhira yetu ya sanaa. Mfano, mitandao ya kijamii, hakuna mtoto atakyeingia katika mitandao, lakini pia kwenye matamasha kama Wasafi Festival pale wanaokuja ni watu wazima, ambao wimbo huu hauna madhara kwao.
Kwenye TV na redio naweza kusema ni sawa kutokana na watoto watakao tazama wimbo huu ila mitandao ya kijamii na kwenye matamasha naomba Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) mkiwa kama walezi wa sanaa mulitazame hili na kuona mnatusaidiaje. Sanaa ni kazi / sanaa ni ajira lakini pia sanaa ni ubunifu asante.
No comments